Karibu Peace by Peace

Peace by Peace ni mwongozo wa ujenzi-amani unaopatikana bure mtandaoni na pia lango lako kuelekea kwa jamii ya kimataifa ya vijana wajenga amani! Hapa, utapata jukwaa shirikishi lililojitolea kushirikisha hadithi, maarifa, na mikakati kutoka kwa vijana wajenga amani duniani kote.

Zuru ramani yetu shirikishi ili kusoma simulizi za moja kwa moja kuhusu juhudi za ujenzi wa amani katika mazingira mbalimbali. Kuanzia mipango ya jamii hadi ushirikiano wa kimataifa, kila hadithi inaangaza (ama kuakisi) njia mbalimbali zinazochukuliwa na watu wenye shauku kama wewe kuifikia amani.

Katika Peace by Peace, tunaamini katika kujifunza kutokana na changamoto za kila mmoja wetu kama vile tunavyojifunza kutokana na mafanikio yetu. Jukwaa hili ni mahali ambapo watu hukutana kubadilishana uzoefu na yale waliyojifunza katika safari ya kujenga amani. Tunakusudia kuimarisha harakati za ujenzi wa amani duniani.

Ikiwa wewe ni mwanaharakati uliyebobea katika masuala ya amani, mwanafunzi mwenye hamu ya kujifunza, au mtu unayetamani kuleta mabadiliko — unakaribishwa kujiunga na jamii yetu maridhawa. Pamoja, tutumie nguvu ya kuungana, kushirikiana, na uongozi wa vijana kuunda dunia yenye amani zaidi!

Peace by Peace ni mwongozo wa kujenga amani unaopatikana bure mtandaoni mahsusi kwa yeyote anayeishi katika jamii iliyogawanyika sana na anayetafakari nini anachoweza kufanya ili kuwa daraja kati ya “sisi na wao”. Tovuti hii inatoa vidokezo vya namna ya kufanya na ushauri kwa yeyote anayetaka kuanzisha mpango wake wa dhati wa kujenga amani. Kwa kadri ya ukuaji wa mradi wa utafiti huu unaoendelea, (tovuti hii) inawaunganisha vijana wajenga amani kutoka mahali popote ulimwenguni na kukuza sauti zao.

Chini ya uongozi wa Dkt. Anne de Graaf (Mhadhiri Mkuu, Uhusiano wa Kimataifa, Chuo Kikuu cha Amsterdam), watafiti wasaidizi wamefanya mahojiano zaidi ya mia moja na vijana wajenga amani, wakichota hekima na uzoefu wao. Tunafanya kazi kwa bidii kuchapisha hadithi na ushauri wao kama nyenzo ya vitendo vya kujenga amani.

Kupitia jukwaa hili, tunalenga kuvuka mipaka ya kijiografia na kuwaunganisha watu wenye shauku ya kuendeleza amani. Tovuti yetu inafanyika kama toleo la kidijitali la mwongozo huu, ikitoa ramani shirikishi ambapo unaweza kutumia kuchunguza simulizi za moja kwa moja kutoka kwa vijana wajenga amani kutoka mabara yote.

Ukiwa kama kijana mjenga amani, mwanafunzi wa chuo kikuu, mtafiti, mtaalamu, au kiongozi wa jamii — unakaribishwa sana kuungana nasi!

Kuhusu Sisi

Using our interactive map

Explore the world of peacebuilding with our interactive map feature! Simply navigate the map and click on the dots marking the locations of peacebuilders to dive into their stories. Every click opens a profile where you can read about their experiences, challenges, and insights.

Contact us

Whether you have a question, or just want to share your thoughts, feel free to contact us. Get in touch via the form, or connect with us through our social media.